
Waombolezaji mbalimbali, Jamaa na Marafiki wameshiriki Shughuli ya Kuaga mwili wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Asembliers City Christian Church (TAG) Upanga jijini Dar es Salaam, Ranwell Mwenisongole aliyefariki hivi karibuni jijini Dar.

Ibada ya Kumuaga Marehemu Mwenisongole inafanyika hivi sasa Katika Kanisa la CITY CHRISTIAN CHURCH (CCC) lililopo Upanga mkabala na Chuo cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam.

Kiongozi huyo aliyefariki karibuni jijini Dar es Salaam na mwili wake utasafirishwa leo kwenda wilayani Mbozi mkoani Songwe kwa mazishi.







