
HAYA ni maajabu ya fungua mwaka! Mchungaji wa kanisa moja nchini Ghana katika mitandao ya kijamii akiwavua nguo wanawake tena kanisani na kuwaogesha na kuwapaka mafuta huku ikidaiwa kwamba kufanya hivyo ni kuwapa upako wa ndoa akina mama hao.
Tukio la aina yake linadaiwa kufanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya, Desemba 31, 2021 kuamkia Januari 1, 2022 kaninani hapo ambapo mchungaji huyo ambaye jina lake bado halijafahamika mara moja, amesema kuwa kuwaosha wanawake ni kuwasafisha, kuwaondolea mikosi na kuwapa upako hivyo kuwafanya wawe watakatifu.
Katika kipande cha video kilichosambaa mitandaoni mchungaji huyo amesikika akiwambia waumini wake (wanawake na mabinti) wajitokeze haraka “kuoga utakatifu” huku wanawake hao wakivua nguo mbele ya mchungaji na kuingia kwenye beseni kubwa wakiwa watupu ili kuogeshwa upako upako huo.
Aidha, mchungaji huyo amesema kwamba anafahamu kuwa kitendo alichokifanya kitazua utata, lakini hana budi kuheshimu maagizo ya Roho Mtakatifu.
Waumini mbalimbali wa dini ya Kikristo kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu tukio la mchungaji huyo huku wakisema kuwa sio maagizo ya Mungu, hivyo anachokifanya mchungaji huyo ni utashi wake binafsi wala haina uhusiano na imani ya Kikristo.
Nini maoni yako kuhusu tukio hilo?