
RAIS Samia Suluhu ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kufuatiwa vifo vya watu 14 waliofariki katika ajali ya barabarani Januari 2, 2022 katika kijiji cha Lidumbe, Wilaya ya Newala mkoani Mtwara.
Taarifa iliyotolewa leo, Ikulu imeeleza kuwa kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Mark Njera chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi wa dereva wa gari aina ya Scania aliposhindwa kulimudu na kuwagonga watu hao na kujeruhi 22.
Aidha, Rais Samia amemtaka mkuu wa mkoa huyo kufikisha salamu za pole kwa wafiwa wote, ndugu jamaa na marafiki na ameungana na familia za wafiwa katika kipindi hiki wanachopitia.
Rais Samia amevitaka vyombo ya usalama barabarani kusimamia na kuongeza juhudi katika kudhibiti ajali za barabarani na kuwataka madereva wote kufuata sheria za usalama barabarani.