
Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kwa namna yoyote ambayo alihisiwa kutoa neno la kumvunja moyo Rais na akavunjika moyo.
Spika Ndugai amesema hayo leo Jumatatu, Januari 3, 2022 wakati akizungumza na wanahabari kufuatia taharuki iliyoibuka mitandaioni baada ya video yake kusambaa ikionyesha kama anapinga tozo.
“Hatukuwa na mazungumzo yote naamini na nakili mitandao sasa hivi ina nguvu limetokea kuwa eti spika anapinga mkopo uliotolewa jambo hili limeniumiza sana kama spika lakini kwenye jimbo letu pia mkopo huo umeweza kutusaidia
“Kwenye ujumbe wangu, hakukuwa na lolote la kudharau juhudi za serikali, serikali ni baba yetu na mama yetu, tunahitaji serikali na tunaiunga mkono na niliwataka wenzangu kujiimarisha kiuchumi, tulipe kodi na tozo, huo ndiyo ulikuwa msisitizo wa hotuba yangu.
“Jambo la kwamba Spika anapinga mkopo wa trilioni 1.3, binafsi limeniuma sana kwa sababu Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ilifaidika na vyumba 112 vya madarasa ambayo ni mazuri sana. Matumizi ya fedha hizi yamekuwa ni mazuri na Bunge tuliidhinisha.
“Sisi Bunge ni sehemu ya hizi fedha Tsh Trilioni 1.3, itakuwa ni dhambi kubwa kuwavunja nguvu viongozi wetu. Tumtie moyo Rais wetu, Tumtie nguvu.
“Kama nimetoa neno lolote la kumvunja moyo Rais Samia Suluhu katika juhudi zake za kuijenga nchi, namuomba radhi sana pamoja na wananchi wote kwa ujumla. Haiwezi kutokea, haitatokea na si rahisi jambo kama hilo kuitokea.
“Nchi nzima inafurahia kwa jinsi mkopo huu ulivyokwenda na uwazi wake. Kwa wale wote walioguswa, niwaombe radhi. Niwahakikishie mimi ni yule yule.
“Nitakua nmechuma dhambi sana kwa mafanikio haya na kazi hiyo hawa wanao katakata clip wasitake kumvunja moyo Rais wetu na kutugombanisha naye, Tumtie moyo Rais wetu Suluhu Samia kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa siku zote akutukanae hakuchagulii tusi,” amesema Ndugai.