
WANAFUNZI 907,803 wanatarajiwa kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza mwaka huu. Akitoa takwimu hizo leo Januari 6 ,2022 Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema idadi hiyo inajumuisha wavulana 439,836 na wasichana 467,967.
Waziri Ummy amesema idadi hiyo imepanda ikilinganishwa na wanafunzi 833,872 waliojiunga kiadato cha kwanza mwaka 2021.
“Uchambuzi unaonesha kuwa mikoa mitano yenye matarajio ya kupokea Wanafunzi wengi zaidi kwa Kidato cha Kwanza ni Dar es Salaam (78,738), Mwanza (68,725), Kagera (50,735), Mara (48,855) na Morogoro (48,515),” amesema Waziri Ummy.
Amesema kuwa orodha ya shule watakazojiunga wanafunzi hao imetolewa na kinachosubiriwa ni muda wa kujiunga na shule.