
Zaidi ya watu 5,000 wamekamatwa nchini Kazakhstan kutokana na maandamano yaliyotikisa taifa hilo la Asia ya kati wiki iliyopita taarifa ya kukamatwa kwa watu hao imetolewa na mamlaka za Khazakhstan leo Jumapili.
Idadi hiyo inaifanya jumla ya wanaoshikiliwa kwa mahojiano kutokana na maandamano hayo kufikia 5,135 taifa hilo lenye takribani raia milioni 19 na utajiri mkubwa wa nishati, limetikiswa na maandamano kwa kipindi cha wiki moja, ambapo watu kadhaa wameuawa.
Kupanda kwa bei ya mafuta ndiko kulikosababisha machafuko katika mikoa ya Magharibi mwa taifa hilo.
Machafuko hayo yalisambaa hadi kwenye miji mikubwa ukiwemo mji muhimu wa kibashara wa Almaty ambako maandamano yaliibuka na polisi walitumia risasi za moto kuwatawanya waandamanaji.