×

ECOWAS Yafunga Mipaka Mali

Mataifa ya Afrika Magharibi yamekubaliana kuiwekea Mali vikwazo vikali ikiwemo kufunga mipaka yao, kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na kuweka vikwazo vikali vya kiuchumi.

Vikwazo hivyo vipya kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi – ECOWAS yenye nchi 15 wanachama vinaonyesha jinsi ilivyoufanya msimamo wake kuwa mgumu kuelekea Mali, ambayo viongozi wa mpito wamependekeza kuandaa uchaguzi Desemba 2025 badala ya Februari mwaka huu kama walivyokubaliana awali na jumuiya hiyo.

Katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano wao wa dharura mjini Accra, Ghana, ECOWAS imesema hatua ya serikali ya kijeshi kuchelewesha utaratibu wa kurejesha utawala wa kiraia haikubaliki kamwe.

Leave a Comment