×
Global Publishers
  • Home
  • Habari
    • Kimataifa
    • Kitaifa
  • Global TV
  • Magazeti
  • Ajira
  • Burudani
    • Audio Music
    • Music Videos
    • Dar Live
  • Michezo
  • Makala
    • Afya
    • Mahaba & Maisha
    • Burudani
    • Hadithi
    • Mikasa
    • Siasa
  1. Home
  2. Habari
  3. Mtuhumiwa wa Mauaji Azidiwa Kizimbani, Jaji Aahirisha Kesi

Mtuhumiwa wa Mauaji Azidiwa Kizimbani, Jaji Aahirisha Kesi

Global Publishers January 15, 2022 4,574 views 0 Comments
SHARE THIS:

Kesi ya mauaji inayomkabili Timothy Gitonga mwenye umri wa miaka 30, anayetuhumiwa kumuua bibi yake, Journes Kiringa mwenye umri wa miaka 80, imeshindwa kusikilizwa kufuatia mtuhumiwa huyo kuzidiwa na maradhi akiwa kizimbani.

 

Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya Embu, nchini Kenya ambapo mtuhumiwa alipoingizwa mahakamani, alianza kulalamikia maumivu makali aliyokuwa akiyahisi, jaji akaamuru kesi iendelee lakini mtuhumiwa aliendelea kulalamikia maumivu makali huku akionesha kuzidiwa.

 

Kufuatia hali hiyo, Jaji Tony Kwambai aliamua kusitisha usikilizwaji wa kesi hiyo na kuagiza mtuhumiwa apelekwe katika Hospitali ya Embu na baada ya matibabu arejeshwe katika Kituo cha Polisi Itabua kisha apelekwe tena mahakamani hapo ifikapo Januari 17, mwaka huu.

 

Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kudaiwa kumshambulia bibi yake na kumuua huku akimjeruhi vibaya babu yake, Jamleck Wamai ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Embu.

 

Tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Rungana, Nembure ambapo sababu za tukio hilo hazijafahamika na baada ya kutenda ukatili huo, mtuhumiwa alitoroka kabla ya kukamatwa na polisi.

SHARE THIS:
Previous Next

Related Posts

Huyu Ndo Demu wa Staa Anayependa Kukaa Uchi! - Global Publishers BURUDANI

Huyu Ndo Demu wa Staa Anayependa Kukaa Uchi!

January 21, 2019
Heineken Silver Kuzinduliwa Kwa Kishindo leo Tanzania - Global Publishers HABARI

Heineken Silver Kuzinduliwa Kwa Kishindo leo Tanzania

June 19, 2025
Fedha Sh 510 Milioni Zapatikana Ujenzi Uzio wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu - Global Publishers HABARI

Fedha Sh 510 Milioni Zapatikana Ujenzi Uzio wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu

June 15, 2025
Habari Kubwa Za Magazeti Ya Tanzania Leo Alhamisi, Januari 11, 2024 - Global Publishers HABARI

Habari Kubwa Za Magazeti Ya Tanzania Leo Alhamisi, Januari 11, 2024

January 11, 2024

Leave a Comment Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

DAKTARI

GLOBAL TV Online




SIMBA
YANGA
NEWS
Global Publishers
  • About Us
Download on the App Store
Get it on Google Play

© 2026 Global Publishers. All Rights Reserved.

Designed by Yatosha Web Services