×

Picha ya Nyani Yamponza Kanye

Shirika la kutetea haki za wanyama la nchini Marekani ‘PETA’ ambalo limetoa taarifa ya kuchukizwa na kitendo cha rapa Kanye West kutumia picha ya nyani aliyechunwa kama “Cover” kwaajili ya wimbo wake mpya alioshirikiana na rapa The Game.

Muda mfupi baada ya Kanye kuzindua wimbo wake mpya “Eazy”, shirika hilo la kutetea haki za wanyama kupitia kwa Rais wake lilitoa taarifa likiwashutumu wawili hao kwa kumtumia nyani aliyechunwa ngozi katika sanaa yao kwa madai ya kuwa si jambo la kiutu.

“Ni nyani wenzetu, na si wa kuwanyanyasa kwa malengo yoyote, si maabara, mbuga za wanyama za barabarani, sinema, au soko la nyama.” alisema rais huyo.

Hadi sasa hakuna yeyote kati ya Kanye na The Game aliyejibu tuhuma hizo licha ya picha hiyo kuendelea kuwepo kwenye kurasa zao za mitandao yao ya kijamii kama tangazo la wimbo wao mpya ‘Eazy’.

Leave a Comment