×

Zoa Zoa Yaendesha Msako wa Kuwanasa Wanaoiga Bidhaa Zake

Dk. Elizabeth Kilili akizungumza na wanahabari ofisini kwake Tabata Segerea, Dar.

 

 

Kampuni ya Grace Products au Zoa Zoa imeingia mitaani nchi nzima kwa lengo la kuwakamata wafanyabiashara wasiyo waaminifu ambao wamekwa wakitengeneza sabuni duni na kuzihifadhi kwenye makasha yanayoonesha zimetolewa na Zoa Zoa.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar mwishoni mwa wiki, bosi wa Grace Products, Dk. Elizabeth Kilili, alisema watu wasiyo waaminifu wamekuwa wakitengeneza sabuni feki za Zoa Zoa Manjanona kuziingiza mtaani, hao ndiyo wanaowindwa usiku na mchana.

Alisema wameshawakamata watuhumiwa kadhaa na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria kwa taratibu nyingine huku wengine wakiingia mitini baada ya kusikia oparesheni hiyo kali na ya kimkakati.

Dk. Elizabeth akionesha bidhaa zake orijino.

 

 

Akasema: “Naomba niwaambie wateja wetu na ndugu Watanzania, ukimkuta mtu anauza sabuni zetu za Zoa Zoa Manjano, ili kuitambua kama ni feki au ndiyo yenyewe, gusa lile neno Zoa Zoa kwenye boksi. Kama Ni feki utaona halina mwinuko, kama ni orijino, lina mwinuko ukigusa.”

Akaendelea: “Hata ile lebo ya Grace nayo ina mwinuko wakati fake hazina hali hiyo. Lakini pia niwaambie wale wanaoendelea au kuwaza kufanya magumashi ya sabuni zetu kuacha mara moja kwani oparesheni yetu siyo ya wazi.” alimaliza kusema Dk. Elizabeth.

Leave a Comment