×

Julio Awatumia Salamu Simba

KOCHA Msaidizi wa Namungo FC, Jamhuri Kiwehlo ‘Julio’ amesema kuwa timu yao ina nafasi kubwa ya kuwapokonya Simba ubingwa wa ligi kuu msimu na huo ndiyo mpango wao.


Julio alifunguka kuwa anasema
hivyo kwa kuwa ana kikosi na timu bora yenye uwezo wa kufanya lolote mbele ya timu yoyote kwenye ligi na ndiyo maana malengo yao msimu huu ni kuwa mabingwa.


Akizungumza na Championi
Jumatatu, Julio amesema Namungo ni moja kati ya timu bora na inayotoa ushindani wa kweli kwenye na ina uwezo wa kuchukua ushindi mbele ya Simba, Yanga, Azam na kila timu na hatimaye kuchukua ubingwa.


“Malengo yetu ni kuchukua ubingwa
wa msimu huu na uwezo wa kuchukua tunao. Namungo ni moja kati ya timu bora sana hapa Tanzania na inawezekana kuchukua pointi tatu kila uwanja.


“Namungo inaweza kuwafunga Simba,
Yanga, Azam na kila timu, hakuna ambacho kinashindikana na ninasema
kuwa Namungo atakuwa bingwa na
hakuna atakayebisha,” alisema Julio.

 

Honour Janza kutoka Burundi alitambulishwa na uongozi wa Namungo kuwa kocha mkuu wa akisaidiwa na Julio na waliisimamia timu hiyo kwenye Mapinduzi na kuondoshwa hatua ya nusu fainali.

Julio awatumia salamu Simba

SABABU TANO KIPIGO SIMBA, MANARA AWAVAA MABOSI SIMBA, YANGA FULL KICHEKO | KROSI DONGO…

Leave a Comment