×

Matetemeko Mawili Yaua Watu 20 Afghanistan

MAOFISA Usalama nchini Afghanistan wamesema watu zaidi ya 20 wamefariki kufikia sasa baada ya matetemeko ya ardhi ya mfululizo kukumba eneo la magharibi mwa Afghanistan siku ya Jumatatu, maafisa usalama walisema.

 

Kwa mujibu wa data kutoka Shirika la Jiolojia la Marekani (USGS), matetemeko hayo ya kipimo cha 4.9 na 5.3 yaliathiri mkoa wa kaskazini-magharibi wa Badghis, ambako na kusababisha nyumba na majengo kuporomoka.

 

Msemaji ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watoto wanne ni miongoni mwa waliopatikana wamekufa kwenye vifusi.

 

USGS ilinakili matetemeko mawili ya ardhi siku ya Jumatatu, ambayo yalipiga takriban kilomita 50 (31mi) kutoka Qala-e-Naw, mji mkuu wa jimbo hilo.

 

Tetemeko la kwanza lilipiga alasiri, na la pili likafuata saa mbili baadaye. Athari zake zilionekana zaidi katika wilaya za Qadis na Mugr.

Leave a Comment