
MNAMO usiku wa kuamkia Jumapili ya Januari 16, 2022 soko la wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga maeneo ya Mchikichini Jijini Dar es Salaam liliteketa kwa moto kwa zaidi ya asilimia 85 na kuacha sehemu kubwa ya soko hilo likiwa majivu matupu.
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais Samia walituma salamu za pole na kuataka wafanyabiashara hao kwa watulivu wakati Serikali ikifatilia kw kina janga hilo.
Wakati wa fukufuku hilo Meya wa jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto amekanusha madai ya Serikali kuhusika kuchoma soko hilo kama ambavyo wengi wanazungumza.
“Hadi ninavyozungumza na ninyi hapa lile soko la Machinga COMPLEX limeshajaa. Ni sehemu mbili ambazo tunakusanya mapato pale Machinga Complex na Mchikichini halafu tuliunguze kwa makusudi kwa mfano tunaamua tuwaondoshe wamachinga tujenge soko maana yake ni lazima tutawatafutia eneo. Mh. Rais Samia Suluhu Hassan alitusisitizia kwamba tukitaka kuwaondosha wamachinga tuwatafutie eneo.
“Mfano mwishoni mwa mwezi huu tutawaondosha wafanyabiashara wa nyama katika machinjio ya Vingunguti hadi sasa hivi tumewaacha pale kwa sababu tunamalizia soko la kisasa la ambalo tunawajengea pale pale na tumelipa fidia Tshs Mil. 520” Omar Kumbilamoto, Meya Jiji la Dar es Salaam.
Matukio ya masoko makubwa hapa nchini kuwaka moto yameshamiri kiasi cha kuibua minongono mingi miongoni mwa watu ambao wengi wamekuwa wakihoji juu ya ufumbuzi wa suala hilo.