×

Kenya Kuingiza Sokoni Mabasi ya Umeme

Kampuni ya kutengeneza vyombo vya moto vinavyotumia umeme nchini Kenya ya Opibus imetangaza kujiandaa kuingiza sokoni mabasi mapya ya umeme yanayotengenezwa nchini Kenya.
Kampuni hiyo inayomilikiwa na Wakenya kwa ushirikiano na Watu wa Sweden imesema hayo yatakuwa Mabasi ya kwanza ya umeme kutumika Afrika na kwamba itaanza na mabasi 10 ya majaribio ambayo yataingia sokoni katikati ya mwaka huu 2022 na yatauzwa kwa gharama ya hadi Ksh milioni 11.3 (sawa na Tsh. Mil 223.738 ).
Malengo ya Opibus ni kuwa na mabasi ya umeme mengi ambayo yatasaidia kupunguza foleni katika Jiji la Nairobi huku yakiwaingizia wamiliki fedha. Mabasi hayo yatakuwa yanachajiwa na kuwa full kwa muda wa saa moja.
Mwezi Desemba mwaka jana Kampuni hiyo ya Opibus ilitangaza pia kushirikiana na Kampuni ya Uber na kusema wataingiza sokoni Pikipiki za Umeme 3,000 ambazo zitarahisisha shughuli za usafiri Kenya.

Leave a Comment