
RAPA nguli Bongo, Farid Kubanda ‘Fid Q’ ametia neno kwenye kile ambacho rapper #Cardib ametweet kupitia akaunti yake ya Twitter kwamba ukiwa mtu maarufu inaboa.
Fid amesema; “Kinachoboa kuhusu umaarufu ni pale ambapo unashindwa kuwa wewe kwa maana ya kuwa labda una-enjoy kula kwa mama ntilie, hauwezi kwa sababu wanaokutazama watakutazama kwa jicho la kwamba umechoka kimaisha kumbe hawajui wewe unapenda msosi wake.
“Muda mwingine unajisikia kujichanganya kwenye magari ya abiria haya (daladala) ukiingia kila mtu anakushangaa umekuja kufanya nini sasa hiyo inaboa.
“Unaweza kuamini kwamba mimi sijawahi kupanda mwendokasi kwa sababu nikipanda mwendo kasi watu watanishangaa kwa nini lakini natamani kupanda, kwa hiyo nimepanga mwaka huu nitapanda mwendokasi na nimewatangazia wajue kabisa.
“Sitojali watanitazama kwa jicho gani maana hiyo imenisababisha nikose baadhi ya starehe, kuna muda umaarufu unaboa kwasababu unashindwa kuwa wewe,” amesema Fid.