×

Mavoko: Wanaofanya Amapiano Bongo Waachwe

STAA maarufu wa Bongo Fleva, Richard Martin Lusinga Rich Mavoko amezungumzia kuhusu muziki wa #Amapiano kuendelea kusikika kwenye soko la muziki wa Tanzania huku akitofautiana na mawazo ya baadhi ya wasanii wanaouponda muziki huo hapa Bongo.

 

Rich Mavoko amesema; “Nafkiri hata hao wanaofanya (amapiano) tusiwawekee mipaka yani kibiashara ukimuwekea mtu mipaka ni kama unamfunga hivi lakini labda kufanya sana ndio inaweza kuwa shida.

 

“Lakini kwa wanaofanya kibiashara haiwezi kuwa shida kwa sababu huwezi kubishana na biashara, ukweli ni kitu ambacho huwezi kupingana nacho.

 

“Hata wao (Wasauzi) wanaulizia kuhusu muziki wao kama umefika huku kwetu ukiwambia umefika wanafurahi maana wao wenyewe wanaupenda na wanaupiga muda wote, nimeenda klabu wanapiga muziki huo tu wao wenyewe wanajipenda sana,” amesema Mavoko.

Leave a Comment