×

Harmonize Akanusha Kuachana na Briana

MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ leo Januari 23, 2022 amebadiliki amebadili maamuzi yake juu ya hali yake ya kimahusiano kwa sasa.

Usiku wa kuamkia Januari 22, 2022 aliandika ujumbe mbalimbali kupitia instagram stori yake kuwa amerudi tena kwenye maisha ya ubachela baada ya kuumizwa kimapenzi.

Harmonize hakuishia hapo alimu-unfollow hadi mpenzi wake Briana jambo ambalo lilifanya watu waamini kuwa penzi lake na mrembo huyo kutoka nchini Australia limefika ukingoni.

Sasa ndani ya masaa 24, Harmonize amebadili maamuzi kaona bora arudi nyumba aliyoizoea kwani kunguni wake ameshawajua kuliko kwenda kuanza upya. Harmonize ametumia ukurasa wake wa Instagram (Instastory) kwa kuandika kuwa

“Sipo Single tuheshimiane“.

Harmonize hakuishia hapo bali amemfollow tena mpenzi wake huyo na hata kwa upande wa Briana ame-mfollow back Harmonize.

Leave a Comment