×

Johari: Mashela yameondoka na ndoa zetu

 

STAA wa kitambo hicho kunako Bongo Movies, Blandina Chagula au Johari anasema kuwa, kipindi kile walichokuwa wakiigiza wamevaa mashela ndipo walijitia nuksi na mashela hayo yakaondoka na ndoa zao mpaka leo hii, maana yeye aliigiza zaidi ya mara tatu kuwa ameolewa na kuvaa shela.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Johari anasema kuwa, amejifunza kitu kikubwa sana katika kuigiza unaolewa na wakati hujaolewa ni kitu ambacho kitakupa nuksi tu maana kwenye ulimwengu wa roho tayari umeshafunga ndoa feki ambayo inazuia ndoa za kweli kuja.

 

“Mashela ndiyo yameharibu kila kitu na hata ndoto za kuolewa kweli kwa sababu inaonekana kiroho tumeshaolewa, sasa kama mimi jamani nimevaa mashela mara tatu hiyo unaichukuliaje sasa kuna ndoa tena hapo? Kwa hiyo nimeseme tu kwamba mashela yameondoka na ndoa zetu,” anasema Johari ambaye amekuwa akitamani kuolewa kwa muda mrefu.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave a Comment