×

Maduka ya Dawa Nje Ya Hospitali Yaondolewe- Waziri Ummy

SERIKALI imewaagiza wamiliki wa maduka ya dawa yaliyopo mita 500 kutoka vituo vya afya nchini kuyaondoa ifikapo Juni 30 mwaka huu.

 

Imeelezwa kuwa maduka hayo yapo kinyume cha kanuni ya famasia iliyowekwa mwaka 2020 hivyo wamiliki watachukuliwa hatua za kisheria.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo Januari 24, 2022 wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga kwa lengo la kuangalia ubora wa utoaji huduma kwa wagonjwa

 

“Nimerudi Wizarani tulitengeneza kanuni maduka yote ya nje ya dawa yanatakiwa kuwa nje umbali wa mita 500 sheria hii niliipitisha kabla sijaondoka Wizarani”

“Maduka yote nawatumia salamu yaliyo ndani ya Mita 500 ndani ya Hospitali Nchi nzima tunakwenda kuyaondoa”

Leave a Comment