
KUTOKA kwenye insta story ya ya supastaa wa Bongo Movies, Jackline Wolper ‘Mama P’ amesema endapo akigundua mwanamke mwingine ametembea na mpenzi wake Rich Mitindo, basi ataachana na mpenzi wake huyo bila kujali mangapi wamefanya pamoja.
Wolper amepost picha yenye maneno haya ‘ata nisikia ulilala nae simuachiii’ na kisha kusindikiza na ujumbe unaosomeka.
“Nilishasemaga huu usemi lakini nimegundua nilikua na njaa hiyo siku sikula vizuri kiukweli kucheatiwa kunauma sana kwa mtu unayempenda nakumuamini nimegundua hiki kitu baada ya mdogo wangu kunambia bwana ake ameweka paswad kwenye sup nikamwambia lazima anakucheat achana nae.
“Sasa vipi me nimkute na mtu tu nisimuache mmh siwezi narudia maneno yangu nikiwa nimeshiba pilau siwezi nitaachana nae siku nikimkuta nauwakika ninao na baada ya week tu nitawatambulisha baba wa kambo,” amesema Wolper.