×

Djuma, Bangala Watimka Yanga

MASTAA wa Yanga, Djuma Shaaban na Yannick Bangala jana Jumanne saa tisa kamili alfajiri walipanda ndege kurejea nyumbani kwao DR Congo tayari kwa kujiunga na timu ya taifa ya nchini kwao.

 

Hiyo ikiwa ni saa chache tangu mastaa warejee jijini Dar es Salaam wakitokea Arusha walipokwenda kuvaana na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Sheikh Amri Abeid mkoani huko.


Katika mchezo huo wa ligi, Yanga
ilifanikiwa kuwafunga Polisi Tanzania bao 1-0 ambalo lilifungwa na Dickson Ambundo akipokea pasi ya Fiston Mayele kabla ya kufunga.

 

Djuma na Bangala wamerejea nyumbani kwao Congo kwa ajili ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya
DR Congo inayojiandaa na mchezo wa
kirafiki dhidi ya Bahrain.


Sasa rasmi timu hiyo itakawakosa
wachezaji wake hao wawili katika mchezo ujao wa Kombe la FA watakaocheza dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Jumamosi hii kwenye

 

Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.Wachezaji hao Jumamosi iliyopita walitangazwa kuwepo katika orodha
ya wachezaji 25 wa timu hiyo
wataokwenda kucheza mchezo huo wa kirafiki.


Nyota hao wawili watakwenda
kucheza mchezo huo maalum wa kujiandaa kutafuta nafasi ya kufuzu
Kombe la Dunia.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Februari Mosi, mwaka huu na wachezaji hao watakuwepo sehemu ya kikosi hicho.


Wachezaji hao tangu wajiunge na
Yanga wamekuwa tegemeo na uhakika wa kuanza katika kikosi cha Nabi
kinachowania Ubingwa wa Ligi Kuu
Bara msimu huu.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

MASTAA YANGA Wachota MIL 265, JEURI ya SIMBA, ETI HAWATISHIKI na POINT | KROSI DONGO..


Leave a Comment