
Muigizaji nyota wa tamthilia ya Ertugrul inayorushwa na kituo cha runinga cha Azam Two, Ayberk Pekcan maarufu kama Artuk Bey raia wa Uturuki amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 51.
Taarifa za kifo cha muigizaji huyo zilitolewa rasmi usiku wa Januari 25 na kutajwa chanzo cha kifo chake ni maradhi ya Saratani aliyopambana nayo kwa muda mrefu.
Taarifa za kifo cha muigizaji huyo maarufu zimewashtua mashabiki wengi hususani wa ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na umaarufu wa nyota huyo baada ya tamthilia ya Ertugrul kutafsiriwa kwa kiswahili.