
MAMA mmoja mwenye jumla ya watoto 10 kutoka kaunti ya Kakamega nchini Kenya aliyejitambulisha kwa jina la Gentrix Wekesa ameeleza masikitiko yake kufuatia mume wake kukataa mambo ya uzaiz wa mpango akishikilia msimamo wake kuwa anataka kuwa na watoto 22.
Bi. Wekesana mwenye umri wa miaka 30, kwa jina Gentrix Wekesa kutoka kijiji cha Navakholo, anatarajia kupata mtoto wake wa 11 hivi kaibuni kwa ni mjamzito, alisema mume wake alikataa kutumia mpango wa kupanga uzazi kwa sababu ya tamaduni.
Akizungumza na TV 47, mama huyo mwenye alisema: “Mimi huzaa hawa watoto kila mwaka. Punde ninapo anza hedhi zangu, napata mtoto mwingine, mdogo bado hajafikisha mwaka mmoja.” Gentrix, ambaye ndiye anategemewa kwenye familia hiyo alisema, amechoshwa na mzigo wa kuwalea watoto hao.
“Ilifikia wakati mmoja ambapo mmoja wa watoto aliacha shule akiwa Darasa la Saba kwa sababu tumeshindwa kumgharamia masomo, akifukuzwa karo ama sare, sikuwa na la kufanya. Wa pili pia amewacha shule. Nilimpeleka mahali asaidie mtu kumchungia ng’ombe na wakati analipwa ananisaidia kuwalea watoto wengine,” alisema mama huyo.
Mume wake, Anthony Wekesa, pia amemzuia kutumia dawa za kupanga uzazi. Hii ni dhana potovu ya kigeni na watoto wachache watamgeuza kuwa kicheko. Aliwahi kujaribu kutumia dawa za kupanga uzazi lakini wakati alifika nyumbani, mume wake alimrejesha hospitalini atolewe.
“Bora anizalie idadi ya watoto ambao mimi nataka. Wanatakiwa wawe watoto,” alisema Anthony. Gentrix aliongezea kuwa mume wake anataka wazae watoto wengi ili wawasaidie katika maisha yao ya mbeleni.