
OFISA Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu ya Yanga, Senzo Mbatha ameweka wazi kuwa kwa moto ambao kikosi chao kinaendelea kuuwasha kwenye Ligi Kuu Bara, wanaamini kuwa ni suala la muda tu kabla hawajatangazwa kushinda ubingwa msimu huu.
Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka sasakwa tofauti ya pointi 10 ambapo wamefanikiwakujikusanyia pointi35 katika michezo yao 13 waliyochezampaka sasa, huku wakiwa wamesaliwa na michezo miwili tu kukamilisha mzunguko wa kwanza ambayo ni dhidi ya Mbeya City na Mtibwa Sugar.
Akizungumzia mipango yao ya ubingwa msimu huu, Senzo alisema:“Tunajivunia mwenendo ambao kikosi chetu kimekuwa nao kwa michezo yote 13 ya kwanza, ni wazi tumefanya kazi kubwa kufikia hapa na binafsi kuona tunaweza kupata matokeo katika michezo migumu ugenini kama vile dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.
“Hili linanionyesha wazi kuwa kwa kiasi kikubwa tuna nafasi kubwa ya kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, nadhani ni suala la muda tu na tunapaswa kuendelea na kasi hii mpaka mwishonimwa msimu.”
Stori: Joel Thomas, Dar es Salaam
SABABU 5 KIPIGO cha SIMBA ni HIZI, KOCHA NABI Asema “SIMBA WASHAUMIA TAYARI” | KROSI DONGO..