×

Chris Brown Akanusha Tuhuma za Ubakaji

HATIMAYE mwanamuzuki Chris Brown ameibuka na kujibu tuhuma za kesi ya ubakaji inayomkabili baada ya mwanamke mmoja kumshtaki na kudai fidia ya dola milioni 20 ambazo ni sawa na zaidi ya Bilioni 46 za Kitanzania.

Kwenye taarifa iliyopita tulikufahamisha kuhusu kesi ya ubakaji anayotuhumiwa nayo nyota huyo baada ya mwanamke aitwaye Jane Doe kudai kufanyiwa kitendo cha ubakaji kwenye boti nyumbani kwa Diddy Miami Star Irland, alipokwenda kwa madai ya kuitikia wito wa Chris brown ambaye alisema kuwa ni rafiki wa kawaida na si mpenzi wake.

Kufuatia shutuma hizo zilizoenea kwa kasi kote duniani, Chris Brown ameamua kuvunja ukimya na kuweka wazi kuwa tuhuma hizo ni kama mpango wa siri unaousukwa kwa lengo la kumdhoofisha kimuziki kwa kuwa si mara ya kwanza kwa yeye kufanyiwa visa vya kutengenezwa vyenye mfumo wa namna hiyo ili kumvurugia kazi zake.

“Kila ninapotoa wimbo mpya wanajaribu kuleta vitu vyao vya kipuuzi” aliandika Chris kupitia ukurasa wake wa mtamdao wa Instagram (Insta Story).

Chris Browm kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘IFFY‘ aliouachia takriban wiki mbili zilizopita huku ukiwa umefanikiwa kupata watazamaji zaidi ya milioni 9 kwenye mtandao wa YouTube.

Leave a Comment