
DUA na sala za kumtakia afya njema mkongwe wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule almaarufu Profesa Jay zimeendelea kumiminika kutoka kwa mastaa mbalimbali Bongo.
Hii ni baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba hali yake kiafya si nzuri na kwamba amelazwa kwenye moja ya hospitali kubwa jijini Dar.
Miongoni mwa mastaa waliompa pole na kumtakia afya njema Profesa Jay ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Mikumi ni Diamond Platnumz aliyemuandikia; “Get well soon prof…”
Gazeti na IJUMAA linaungana na wote wanaomuombea Profesa Jay apone haraka ili aendelee kutoka burudani kwa mashabiki wake.
Profesa Jay ni mmoja wa waasisi wa muziki wa Kizazi Kipya nchini ambao kwa sasa unaajiri vijana wengi na kuwapa mkate wa kila siku.