×

Wateja wa Vodacom M-Pesa Kuvuna Gawio la Tzs 3.4 Bilioni Kutoka kwa Miamala ya Pesa

Mkurugenzi wa M-Pesa Bwana Epimack Mbeteni.

 

 

28 Januari 2022, Dar es salaam: Kampuni ya teknolojia na mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania PLC leo imetangaza kuwa itatoa jumla ya TZS 3.4 bilioni ikiwa ni gawio kwa wateja wake wa M-Pesa ambao wametumia huduma hiyo robo ya nne ya mwaka huu (Oktoba hadi Disemba).

 

Akiongea juu ya hili, Mkurugenzi wa M-Pesa Bwana Epimack Mbeteni alisema kuwa faida italipwa kwa wateja wote, mawakala wa rejareja na washirika wengine wa biashara wa M-Pesa ambao watapokea malipo kutokana na huduma ya malipo waliyofanya kupitia simu zao za mkononi.

 

“Huduma yetu ya pesa kupitia simu za mkononi, M-Pesa, inaendelea kuwa hadithi ya mafanikio ya kushangaza, ikitoa thamani kubwa ya kijamii na kifedha kwa Watanzania.

 

Tumeona ukuaji mkubwa kwenye jukwaa la M-Pesa na wateja zaidi, mawakala, wafanyabiashara na taasisi zinazofanya biashara kufikia karibu TZS bilioni 100 kila siku.

Leave a Comment