×

Kijana Akataa Milioni 11 za Bilionea Namba 1 Duniani

KIJANA mwenye umri wa miaka 19 aitwae Jack Sweeney amekataa ofa ya dola za Kimarekani 5000 ( sawa na Tsh. Milioni 11.5 ) kutoka kwa Tajiri namba moja Duniani Elon Musk ambaye yupo tayari kumlipa ili aifute akaunti feki ya twitter inayotweet safari za Ndege binafsi ya Bilionea kila inapopaa.

 

Akaunti hiyo ambayo Jack ameipa jina la Elon Jet ina followers zaidi ya 150,000 na huwa ina-tweet kila Private Jet hiyo inapopaa na kutua pamoja na muda ambao inatumia iwapo angani.

 

Jumbe zilizosambaa mtandaoni zinaonesha bilionea Elon akiwa amemtumia Jack akimuomba aifute akaunti hiyo kwa sababu ina hatarisha usalama wa Elon na akamuahidi pia kumpa fedha ambazo zitamsaidia kwenye masomo na vitu vingine.

 

jack kwa upande wake amekataa ofa ya Elon na kusema fedha hiyo ni ndogo ukilinganisha na furaha anayoipata kwa kuwa moyo wake unapata raha kwa kufanya anachokitaka na kusema raha hiyo haiwezi kununuliwa kwa fedha. Jack amemshauri Elon kutafuta program itakayomsaidia kublock ndege yake isiwe inafuatiliwa.

 

“Inaonekana Elon Musk ameufanyia kazi ushauri wangu na anatumia hizo program napata shida kum-track lakini bado hawajaweza kunizuia,” amesema Sweeney.

Leave a Comment