×

Tanga: Watano Wauawa Mapigano ya Wakulima na Wafugaji

MKULIMA Richard Masaki amesema waliona vijana jamii ya kimasai wakiingia katika eneo lao na kuanza kuwashambulia, kwa kuwapiga na baadae yakaanza mapigano ya mapanga na risasi hadi kutokea vifo hivyo.

 

Aidha mfugaji David Kimaki amesema ampoteza mjukuu wake Betina ambae ameuwawa kwa kukatwa na Panga katika shambulio hilo.

 

“Tulivyopita mbele kidogo tukashambuliwa kwa risasi, nikajua ni wale wale watu nikachukua hatua nikampigia OCD kumpa taarifa kwamba huku kuna mauaji mengine, tukaongozana na kuona miili mingine zaidi”, amesema Kimaki.

 

Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama akiwa eneo la tukio licha ya kuongoza zoezi la kukusanya miili ya marehemu amesema watu watano wamefariki dunia na watutu kujeruhiwa, kutokana na tukio hilo.

 

Aidha amezitaka pande zote mbili kusitisha mapigano na kusalimisha silaha zao ili utatuzi wa mgogoro huo ufanyike kwa njia ya amani kwani njia wanayotumiwa hawawezi kupata utatuzi.

 

“Wito ninaotoa kwa pande zote mbili zinazozingamana hapa ni kuacha mapigano haya haraka, kwani mapigano haya hayawezi kusaidia katika kutafuta ufumbuzi na waweke silaha zao chini”, amesema DC Busalama.

Leave a Comment