×

Vijana Watakiwa Kuchangamkia Shindano la Kujilinda HIV na Uzazi wa Mpango

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Dkt International Tanzania, Farida Lubanza.

 

 

 

Vijana hapa nchini wametakiwa kushiriki shindano la Cycle For HIV 2022 ili kulinda afya zao kwa kuonesha uelewa wa kujilinda na virusi vya HIV pamoja na mimba zisizotarajiwa.

Akizungumza na wanahabari Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Dkt International Tanzania, Farida Lubanza inayozalisha vidonge vya uzazi wa mpango na kondom amesema shindano hilo limeandaliwa kiutofauti na kampeni zingine kama hizo lengo muhimu likiwa kubadili mienendo ya vijana katika kujilinda ili wasipate maambukizi ya ukimwi pamoja na mimba zisizotarajiwa.

“Suala la uzazi linatakiwa kuwa suala la mtu kulipenda na kuepuka mimba zosizotarajiwa.

“Hivyo shindano hili tumeliweka kiburudani zaidi ambapo litaambatana na mbio za baiskeli kule Zanzibar litakapofanyika lengo likiwa ni kulinda afya maana hayo yatakuwa ni mazoezi muhimu ya kulinda afya” amesema Lubanza.

Waandaaji wa shindano hilo pichani walipokuwa wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

 

 

 

Jinsi ya kushiriki shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Kisiwani Zanzibar Februari 18 mpaka 20 mwaka huu 2022, Lubanza amesema unachotakiwa ni kupitia mitandao yao ya kijamii.

Ameendelea kusema mshiriki wa shindano hilo unatakiwa kuwa na afya njema kwakuwa kutakuwa na mbio za baiskeli ambazo zitakuwa na urefu kidogo.

Kigezo kingine alichotoa ni lazima mshiriki awe raia na mkazi wa hapa nchini Tanzania.

Lubanza amewataka wanaopenda kushiriki shindano hilo kupitia page zao tatu ambazo ni Bull condom, Fiesta condom tz na Kiss condom tz na akishafanya hivyo apige picha ambayo ataweza kuipakia kwenye page yake binafsi huku akitutag page zetu zote tatu.

Lubanza ameendelea kusema akishafanya hivyo atumie hash tag ambayo ni Cycle For HIV 2022 na awatag rafiki zake watano.

Mwisho wa kujisajili katika shindano hilo ni Februri 7 mwaka huu 2022 ambapo baada ya hapo kutakuwa na jopo la majaji ambalo watachagua washindi wanne ambao watatangazwa Februari 11 mwaka huu 2022.

Leave a Comment