
Siku ya Alhamisi, mwigizaji “Arnold Schwarzenegger” alishiriki picha ya filamu yake mpya “Zeus” kwenye Instagram ambapo alionekana amevaa kama miungu ya kigiriki. Akiacha nukuu kwa kuandika, “Inakuja Februari 2022.”
Gavana huyo wa zamani wa California ameendelea kujishughulisha na kazi kwenye filamu za Hollywood na miradi mingine kama vile Kung Fury 2, Triplets na The Legend of Conan.
Ikumbukwe hayo yote yanakuja baada ya wiki iliyopita, Schwarzenegger aliporipotiwa kuhusika katika ajali ya magari iliyosababisha mwanamke mmoja kujeruhiwa, jarida la People lilithibitisha hilo.
Muendelezo wa filamu za Terminator na Comando ni baadhi ya filamu pendwa zaidi toka kwake Arnold, ambazo zilimpa jina kubwa na mashabiki wengi waliotokea kumpenda zaidi na kukubali kazi zake.