×

Kimbunga Ana Chaua Zimbabwe

Watu kumi wamefariki dunia nchini Zimbabwe baada ya kusombwa na maji walipokuwa wakijaribu kuvuka mto uliokuwa umejaa karibu na mpaka na Msumbiji.

Hivi ni vifo vya kwanza kutangazwa nchini humo kutokana na kimbunga Ana, ambacho imeua zaidi ya watu 80 katika nchi nyingine za kusini mwa Afrika.

Zaidi ya watu 100,000 pia wamekosa makazi katika nchi za Madagascar, Malawi na Msumbiji kutokana na mafuriko makubwa.

Maafisa nchini Zimbabwe wanasema nyumba, mazao, madaraja na shule pia zimeharibiwa. Kimbunga kingine cha kitropiki kinaelekea eneo hilo.

Kimbunga cha Batsirai kinatarajiwa kutua Madagascar siku ya Jumamosi ikiwa na upepo unaozidi kasi ya 200km/h (124mph).

Leave a Comment