
WAKATI Diamond Platnumz akiendelea kutrendi na Zuchu kwamba ni wapenzi, baby mama wa jamaa huyo naye ameona asibaki nyuma hivyo amevunja ukimya na kidume.
Kuhusu Diamond na Zuchu, mtu wa karibu wa familia ya Wasafi, Juma Lokole ndiye alithibitisha wawili hao kuwa wapenzi tangu mwezi uliopita waliponaswa wakijiachia hotelini jijini Dar.
Ishu hiyo imekuwa ikimuweka Tanasha kwenye wakati mgumu kwani baadhi ya mashabiki wake waliamini yeye na Diamond wangerudiana ili wamlee mtoto wao, Naseeb Junior na kupata watoto wengine.
Hata hivyo, kwa hali ilivyo, anaona jambo hilo haliwezekani tena hivyo Tanasha ameamua kuvunja ukimya na kuachia picha akiwa na mwanaume ambaye hajulikani mitandaoni ikielezwa ni namna ya kujibu mapigo na kujipooza.