
Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) mapema Feburuari ilifanya semina na waandishi mbalimbali wa habari wa hapa nchini, katika ukumbi wa Edema,uliokuwepo Mkoani Morogoro.
Semina hiyo ambayo itakuwa ni ya siku mbili ni kuhusiana na kuwapa uwezo zaidi wasichana balehe na wanawake vijana, ambao katika takwimu zinaonyesha kuwa ndio wenye maambukizi makubwa kwa sasa ambao ni kuanzia umri wa 15-24.

Katika semina hiyo pia walizungumzia kuhusu mpango 95-95, ambapo unaonekana wazi kutimizwa kutokana na baadhi wa watu wengi wamejitambua tayari na wameanza ipasavyo kutumia dawa na wameshafubaza VVU na huku takwimu ikionyesha kuwa watu milioni 1.7 tayari wana maambukizi ambapo ni sawa na asilimia 4.8 huku mkoa wa Njombe ndio ukiongoza kwa maambukizi makubwa ya 11.4 na mkoa wenye maambukizi madogo kabisa nchini ni Lindi ambao ni 0.3.
Habari Imelda Mtema