×

Ratiba ya Kukatika Umeme Februari 6, Hii Hapa

Shirikal la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Rukwa, limetoa taarifa ya kukatika umeme kesho Februari 6, 2022 kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 1:00 usiku ili kupisha matengenezo ya dharura katika kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo Mbala katika Nchi jirani ya Zambia.

 

Njia ya umeme itakayoathirika ni Kabwe Pensulo Line (330 KV) Zambia na maeneo yatakayoathirika ni baadhi ya maeneo ya Sumbawanga.

Mjini, Wilaya yote ya Nkasi , Wilaya ya Laela (Sumbawanga Vijijini) Wilaya ya Kalambo na Halmashauri ya Mpimbwe “Tafadhali usishike wala kukanyaga waya ulioanguka /kukatika”

Leave a Comment