×

Nabi Amchomoa Kaseke Yanga

 

BAADHI ya mastaa wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu ni pamoja na Deus Kaseke ambapo inatajwa kuwa uongozi wa klabu hiyo hauna mpango wa kumuongezea mkataba kutokana
na kushindwa kuonesha makali
yake chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.


Kaseke ambaye alikuwa na
kiwango kizuri msimu uliopita wa 2020/21, msimu huu mambo yamekuwa magumu kwake ambapo ameshindwa kumshawishi kocha Nabi kumuanzisha kwenye kikosi chake.


Chanzo kutoka ndani ya Yanga,
kimeliambia Spoti Xtra kuwa:
“Kuna baadhi ya wachezaji wa
Yanga mikataba yao inaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu wakiwemo Saidi
Ntibazonkiza ‘Saido’ na Deus
Kaseke.


“Saido uongozi upo tayari
kumuongezea mkataba kutokana na kiwango chake kuwa bora, pia kocha Nabi (Nassredine) amesema bado anamuhitaji kwenye kikosi chake.

 


“Jambo zito lipo kwa Kaseke
ambaye msimu uliopita  aliongezewa mkataba wa mwaka lakini ameshindwa
kuonesha kiwango bora kiasi
cha kuwashawishi viongozi na benchi la ufundi.


“Viongozi kwa sasa
wamesema hawana mpango wa kumuongezea mkataba wa kuendelea kubaki kwenye timu
lakini pia kuna uwezekano wa
timu kuachana na Paul Godfrey ambaye kwenye dirisha dogo alikuwa kwenye orodha ya kuachwa.”

Leave a Comment