×

Vodacom “Shangwe Lipo Palepale” Yatoa Zawadi za Ada kwa Washindi 10 Mbagala, Dar

Meneja wa Mauzo Vodacom kanda ya Dar es Salaam, George Nyanda akizungumza na wakazi wa Mbagala wakati wa makabidhiano ya zawadi mbalimbali kwa washindi wa promosheni ya Shangwe Lipo palepale iliyofanyika viwanja vya stendi ya mabasi Mbagala.

 

 

 

AKIZUNGUMZA kwa niaba ya wenzake mmoja kati ya washindi aliyejishindia ADA ya shule kwa watoto wake, Jackline Macha mkazi wa Kibamba alisema “kwa kweli sikuweza kuamini mara nilipopigiwa simu kutoka Vodacom nikiwa kwenye shughuli zangu  za kila siku na kuambiwa umejishindia zawadi kutoka Vodacom, nilifurahi sana kwa kuwezesha kunipunguzia mzigo huu wa ADA mwaka huu ambao kwangu  ulikuwa mkubwa sana” .

Nawashukuru sana Vodacom kwa zawadi hii na naomba nitoe wito kwa watanzania watumie mtandao wa vodacom kupitia huduma yake ya Mpesa kila mara.

 

Nae Meneja wa Mauzo Vodacom kanda ya Dar es Salaam, George Nyanda alisema ” Hii ni fursa kwa watanzania kujishindia zawadi mbalimbali kupitia promosheni yetu ya Shangwe Lipo palepale, ambayo tumeianza mwezi Novemba mwaka jana kama “Show Love Tule Shangwe” kwa kuwapatia wateja wetu zawadi wewe na umpendae kwa msimu wa sikukuu ya Christmass na mwaka mpya na sasa tumeenda mbali zaidi kwa miezi hii ya mwanzoni mwa mwaka tumeamua kutoa ADA ili ziweze kuwasaidia wazazi na walezi kupata nafuu ya watoto wao waweze kwenda shule bila tatizo”. alimaliza kusema Nyanda.

Jumla ya washindi kumi wa Ada, washindi kumi wa simu na washindi wanne wa Tv walipatikana, ili uweze kujishindia zawadi unatakiwa kutumia huduma ya M-Pesa kwa kutuma na kupokea pesa, kufanya malipo kwa M-pesa kwa kupitia namba *149*01#

Leave a Comment