×

Kabwili Yupo Zake Tabata FC

BAADA ya kutoonekana ndani ya kikosi cha Yanga kwa muda mrefu, golikipa Ramadhan Kabwili, ameonekana
akicheza fainali
ya Kombe la Ng’ombe akiwa na Tabata FC.


Kabwili ambaye
aliondoka kambini tangu Yanga ilipokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo uliochezwa Novemba 20, 2021, mpaka leo hajaonekana akiwa na kikosi hicho kinachonolewa
na Kocha Mkuu, Nassredine
Nabi.


Juzi Jumapili, Spoti Xtra
lilimshuhudia kipa huyo akiwa kwenye kikosi cha Tabata FC ambacho kilicheza
mchezo wa fainali ya
kombe la Ng’ombe dhidi ya Tabata Future kwenye Uwanja wa Tabata Shule uliopo Tabata jiji Dar.


Mchezo huo
ulimalizika kwa Tabata FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuchukua zawadi ya ng’ombe huku Tabata
Future wakiambulia
mbuzi wawili ambao ni zawadi ya mshindi wa pili.

STORI NA LEENESSAU, DAR

UCHAMBUZI: GSM KUJITOA UDHAMINI LIGI KUU, UTATA WA MKATABA WAIBUKA…

Leave a Comment