
MIDOMO wazi! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia nguli wa muziki wa Bongo Fleva, H. Baba ambaye wengi wanamuona kwenye nafasi ya uchawa kwa msanii Harmonize, kuamua kuhamia kwa Diamond Platnumz mtu ambaye alikuwa akimkosoa kila mara.
Ukiachana na issue ya kumpost kwa sana Diamond kwenye account yake ya Instagram, H. Baba amem-Unfollow Harmonize na ku-mfollow Diamond na kisha kumu-unfollow tena.
Wengi wamehusisha tukio hilo na orodha ya wasanii aliowaanika Harmonize kuwa watakichafua kwenye tamasha la Harmonize la Afro East Carnival, Machi 5, mwaka huu, wakati kwenye orodha ya wasanii hao, H. Baba hayumo. Kitendo kinadaiwa kuwa inawezekana kikawa kimemuumiza H Baba na ukizingatia ni mtu aliyempigania sana Harmonize mitandaoni.
Mbali na hilo, H Baba pia ameamua kuweka wazi hisia zake za kuamua kum-post Diamond Platnumz kwa kueleza kuwa amefanya hivyo bila kushawishiwa na mtu yoyote, na yeye si chawa bali ni shabiki mkubwa hivyo akikubali kitu hujitoa kufa na kupona.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa H Baba, ameposti video kadhaa za Diamond na kuandika; “Mnatakiwa mjifunze mimi ninamaisha yangu binafsi nimeridhika nayo sina ninacho nichakwangu sijashawishiwia namtu yoyote KUMPOST Simbaaa @diamondplatnumz ni mimi mwenyewe nakihelehele changu.
“Kama anafanya poa kwanini nisimpost waswahili wanasema maneno kibao narudia MSUKUMA hanunuliwi wala hanunuliki ata sikumoja mimi sio muajiliwa wa mtu ni mwanamuziki pia nishabiki kama mwanamuziki mwenzangu kaupiga mwingi nisiseme nasema kwa hili @diamondplatnumz kaupiga Mwingi…
“Umeuwaaaaaah ATI nini Ameuwaaaah ATI niniiii Ameuwaaaaah jeshi la mtu mmoja ndio mimi #rais wa insta ndio mimi @h.baba_ wengine fake fake kosa langu ni kihelehele changu mwenyewe page ni yakwangu sipangiwiiiiiiii. mimi sio chawa mimi nishabiki mkubwa nikikubali nimekukubali kutoka moyoni najitoa kufa au kupona.”
Hata hivyo wengine wamechukulia ni kama kiki ili kuli-boost Tamasha hilo la Harmonize na si kwamba H Baba aanamfagilia Mondi ama kumpondaq Harmonize.