×

Mwanaume Aliyevunjika Uti wa Mgongo Aanza Kutembea

MWANAMUME aliyepooza baada ya kukatika uti wa mgongo ameweza kutembea tena, kutokana na kipandikizi kilichotengenezwa na timu ya watafiti wa nchini Uswizi.

Ni mara ya kwanza mtu ambaye amekatwa kabisa uti wa mgongo kuweza kutembea bila msaada. Teknolojia hiyo hiyo imeboresha afya ya mgonjwa mwingine aliyepooza kiasi kwamba ameweza kuwa baba.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la Nature Medicine. Michel Roccati alikuwa amepooza baada ya ajali ya pikipiki miaka mitano iliyopita. Uti wa mgongo wake ulikatwa kabisa na hakuwa na hisia hata kidogo katika miguu yake.

Lakini sasa anaweza kutembea kwa sababu ya upandikizaji huo ambao umeunganishwa kwa njia ya upasuaji kwenye mgongo wake.

Leave a Comment