×

Yanga Yaitengea Mtibwa Siku 15

KIKOSI cha Yanga, kimeitengea Mtibwa Sugar siku 15 za kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika
mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa
kuchezwa Februari 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Manungu,
Morogoro.


Yanga wametamba kuwamaliza
Mtibwa wakiwa kwao huku wakiwa na kumbukumbu ya kuishuhudia Simba
ikitoka suluhu ilipokwenda kucheza huko
hivi karibuni.


Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara hivi
sasa, Yanga wanaongoza wakiwa na pointi 36, huku Mtibwa ikiwa na pointi 12 katika nafasi ya 14. zote zimecheza mechi 14.


Akizungumza na
Championi Jumatano, Winga wa Yanga, Dickson Ambundo, amesema: “Maandalizi yetu
yapo vizuri kuelekea mchezo huo, tumepata
muda wa kupumzika wa kutosha, sasa ni muda wa kujipanga kuwamaliza Mtibwa.

 

“Kwaupande wangu nimejipanga kupambana kwa hali ya juu ili kuweza kuisaidia timu yangu kupata matokeo
mazuri, ukiangalia tulipata matokeo ya
sare kwa mchezo uliopita na mchezo huu  tunataka matokeo ya ushindi.

Stori: Careen Oscar, Dar es Salaam

Leave a Comment