×

Jux: Sijawahi Kumfollow Harmonize

STAA wa Bongo Fleva, Juma Jux amesema kuwa hajawahi kum-follow mwanamuziki mwenzake Harmonize ambaye ni CEO wa Lebel ya Konde Gang katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

 

Kauli hiyo ya Jux ambaye ni CEO huyo wa African Boy’ kumpiga Unfollow Harmonize imekuja ikiwa ni siku mbilii baada ya kutokea sintofahamu kufuatia Harmonize kuachia orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye shoo yake ya Afro East Carnival huku miongoni mwa wasanii hao akiwataja Jux na Darasa.

 

Hata hivyo waasanii hao walimtaka ayatoe majina yao kwani hakukuwa na makubaliano kabla ya kufanya kitendo hicho. Harmo alionyesha kuchukizwa na kauli hizo na kuamua kuifuta post hiyo kisha kuweka post nyingine yenye orodha ya majina ya wasanii watakaopanda jukwaani ambayo haikuwa na majina ya Darasa wala Jux.

 

Mbali na hilo pia mkali huyo anaefanya poa kwa sasa na wimbo wake wa ‘I Love You’ kupitia amesema kwamba  hata supastaa wa Bongo, CEO wa WCB Diamond Platnumz amem-follow sikuhiz za hivi karibuni, takribani mwezi mmoja uliopita.

Leave a Comment