×

Nanai Ajiuzulu TPSF

Francis Nanai ameachia nafasi yake ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) akiwa ametumikia nafasi hiyo kwa karibu miezi 14.

Nanai aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL) aliteuliwa Disemba 2020 baada ya mtangulizi wake, Godfrey Simbeye kutangaza kujiuzulu mwezi Machi, 2020.

Taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa TPSF, Angelina Ngalula imesema Nanai alijiuzulu Februari 8, 2022
Katika kipindi cha Mpito, Bodi imemteua Raphael Laizer kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji kuanzia Februari 9, 2022.

Leave a Comment