×

Poshy Queen: Kuzaa Kumeniongezea Urembo

MWANAMAMA ambaye alipata umaarufu kutokana na umbo lake matata la nyingu kwenye mitandao ya kijamii Bongo, Jacqueline Obedi almaarufu Poshy Queen anasema kuwa, tangu amejifungua mtoto wake wa kwanza, amezidi kuwa mrembo, tofauti na hata alipokuwa hajajifungua.


Akizungumza na
Gazeti la IJUMAA, Poshy anasema kuwa, watu wengi wanadhani unapopata mtoto, basi mwili unaharibika, lakini ukweli ni kwamba ukizaa na ukajikubali mwili unakuwa mzuri na unaongezeka mvuto.


“Tangu nimejifungua
kwa kweli siku hadi siku naona kabisa mvuto umeongezeka sana, maana wengine walikuwa wanasema nikijifungua nitaharibika, lakini ukweli ni kwamba tangu nijifungue nimezidi kuwa bomba sana na
ninavutia tu tofauti hata
na mwanzo,” anasema Poshy ambaye ni mama wa mtoto mmoja.

Stori; Imelda Mtema, Dar

KISA UBINGWA YANGA WASHTUKIA, WAMUONYA MAYELE, SIMBA WAANIKA SIRI ZA KUWAUWA ASEC MIMOSAS ..

Leave a Comment