
Bibi wa miaka 100, Jane Kibondo mkazi wa kijiji cha Kwambe kata ya Dumila amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga kwa kumsaidia kurejeshewa Shamba lake zaidi ya hekari 6 analodai kudhulumiwa na aliyekua mwenyekiti wa Kijiji hicho, Mkunda Yohana.
Hivi karibu Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alahj Majid Mwanga alipokea ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa mjukuu wa Bibi huyo ukieleza namna walivyodhulumiwa Shamba hilo na Bwana Mkunda Yohana kwa kuliuza kwa watu mbalimbali bila ridhaa yao.
Baada ya kupata ujumbe mfupi kutoka kwa mjuku wa bibi huyo akalazimika kufika katika eneo Hilo ili kufahamu ukweli wa tukio hilo.
Ambapo kwa mujibu wa maelezo aliyoyapokea kutoka kwa kikongwe huyo na kujiridhisha DC Mwanga akaiagiza serikali ya kijiji kumsaidia bibi huyo kurejeshewa eneo lake.
DC Mwanga amekua na utaratibu wa kutoa namba ya Simu kwa wananchi wote wa Wilaya hiyo katika mikutano yake ya hadhara ili kutoa nafasi kwa wananchi wanaoshindwa kufika katika ofsi yake kutoa malalamiko badala yake malalamiko yao wanafikisha kwa njia ya ujumbe mfupi au kupiga Simu .