×

Jina la Mtoto wa Kylie na Travis Laanikwa

Mrembo maarufu duniani na mfanyabiashara kutoka familia ya Kardashian, Kylie Jenner na mzazi mwenzake ambaye ni staa wa muziki dunia Travis Scott wamempa jina la Wolf Webster mtoto wao kiume waliyempata hivi karibuni. Mtoto wa kwanza aliitwa Stormi Webster.

 

Travis Scott ambaye jina lake kamili ni Jacques Bermon Webster alijipa jina la Travis Scott kwa kuchukua jina la mjomba anaeitwa Travis na kuunganisha na jina la Scott kutoka kwa mwanamziki aliyekuwa anampenda sana Kid Cudi ambaye jina lake kamili ni Scott Mescudi.

Leave a Comment