
Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mchezaji wa Ruvu Shooting, Ally Mtoni Sonso umepumzishwa katika makazi yake ya milele hii leo Februari 12, 2022.

Sonso alifariki Dunia siku ya Jana, Februari 11 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na tatizo la mguu lililokuwa likimkabili.

Sonso amezikwa katika makaburi ya Magomeni Kondoa. Sondo ameacha simanzi kubwa kwa wachezaji wenzake, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa soka kote nchini.

Kipindi cha uhai wake, Sonso aliwahi kucheza katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ pamoja na vilabu kadhaa ikiwepo Lipuli FC, Yanga SC, KMC, Kagera Sugar pamoja na Ruvu Shooting.

Tazama hapa chini maziko ya Mchezaji huyo jioni ya leo, Jijini Dar es Salaam ambapo viongozi wa Klabu mbali mbali na Rais wa TFF, Wallace Karia walihudhuria mazishi ya mwanandinga huyo.

Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani Ally Mtoni Sonso.