
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha kuwezesha wajasiriamali cha Station F Start Up Roxanne Varza pamoja na Meneja Mawasiliano wa Kituo hicho Grégoire Martinez kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa Kituoni hapo ikiwemo kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata elimu ya ubunifu wa kibiashara, fursa za mitaji yenye masharti rafiki pamoja na masoko.
Rais Samia amefanya mazungumzo hayo leo Februari 12,2022 alipotembelea Kituo hicho Paris nchini Ufaransa.