
MKUU wa Wilaya ya Temeke jijini Dar, Jokate Mwegelo amesema tayari wameunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha kuungua kwa Soko la Mbagala, Rangi-Tatu usiku wa kuamkia leo Februari 13, 2022.
“Tumeunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha moto na tumeipa siku tatu hadi nne, kikubwa tumetoa maelekezo kwa manispaa Kamati ya uchunguzi ikimaliza kazi wafanyabiashara waruhusiwe kurudi sokoni kufanya biashara huku ikiwekwa mipango ya kukarabati na kuboresha soko hilo.
“Uharibifu haukuwa mkubwa sana kwa sababu tumeweza kuuwahi moto mapema kabisa, tumezima moto kwa wakati kwa sababu eneo lilikuwa wazi na magari ya Zimamoto yakapita kwa urahisi kwa hiyo tunaendelea kusisitiza watu watoke barabarani kwa sababu tunaona faida kama hizo magari yamepita bila stress.
“Kamati ya uchunguzi wa chanzo cha soko kuungua inaendelea na kazi na itatupa majibu ndani ya siku tatu hadi nne, lakini niwaombe watu wakimaliza biashara zao wahakikishe wamezima vizuri umeme na majiko, wahakikishe wamepanga vitu vyao vizuri ili kupunguza risk za moto,” amesema DC Jokate.