
RAIS wa Algeria Abdelmadjid Tebboune amesema, serikali yake itaanza kutoa malipo ya dola 100 za kimarekani ambayo ni zaidi ya shilingi 200,000 za Kitanzania kila mwezi, pamoja na baadhi ya huduma za matibabu kwa vijana wasio na ajira wenye umri wa kuanzia miaka 19 hadi 40.
Rais Tebboune, amewaambia waandishi wa habari kwamba malipo hayo yataanza mwezi Machi hadi pale mhusika atakapopata kazi.
Akitoa tangazo hilo Rais Tebboune amesema kuwa, Algeria ndio nchi ya kwanza nje ya bara la Ulaya kuanzisha mfumo huo, na kuongeza kuwa sasa kuna zaidi ya watu laki sita wasio na ajira nchini Algeria.